KARIBU UWESESCO - SKULI YA SEKONDARI YA UWELENI; P.O.BOX 100; TEL: +255 24 245 6182; EMAIL: uwesesco@gmail.com ;WEB: http://uwesesco.blogspot.com UWELENI MKOANI PEMBA...

Historia ya Shule ya Uweleni

Katika ukurasa huu mpendwa msomaji utapata fursa ya kuijua historia ya Skuli ya Uweleni kwa ufupi:


HISTORIA FUPI YA SHULE YA UWELENI:

Shule hii ipo MKOANI karibu na HOSPITALI YA ABDALLAH MZEE ni wastani wa kilomita moja (1km) kutoka bandari ya MKOANI kuelekea CHAKE CHAKE.

Shuke ya uweleni imeanzishwa (imefunguliwa) mwaka 1932 na ilijuilikana kwa jina la MKOANI GOVERNMENT SCHOOL chini ya uongozi wa ABDALLAH SADALA akiwa ni mwalimu mkuu wa mwanzo.

Mwaka 1959 shule hii ilifanywa kuwa ni ya wavulana pekee na hivyo kubadilishwa jina na kuitwa MKOANI BOYS SCHOOL.Mwaka 1969 ilifanywa tena kuwa skuli ya mchanganyiko wa wanafunzi wanaume na wanafunzi wa kike na hivyo pia kubadilishwa jina na kuitwa SKULI YA UWELENI, mwaka huo huo wa 1969 shule hii ilibahatika kupandishwa daraja na hivyo kufunguliwa Sekondari Ya Awali.

Mwaka 1988 shule hii ilipandishwa tena daraja na kuwa shule ya sekondari tu, baada ya kufunguliwa darasa la 12 (FORM IV) na hivyo pia kubadili jina lake na kuitwa UWELENI SECONDARY SCHOOL.

Mwaka 2005 shule hii ilipandishwa tena daraja na kuweza kutoa elimu ya juu ya kidato cha tano na sita (FORM V AND FORM VI) Advanced Level Education ikiwa ni shuke pekee ya kiwango hicho kwa wilaya ya MKOANI chini ya uongozi wa ndugu SHEHE HASSAN MOH’D ambaye ndiye kiongozi wa shule hii hadi leo.

Mwaka 2012/2013 SHULE YA SEKONDARI YA UWELENI imebahatika kufanyiwa ukarabati mkubwa (major repair) wa majengo yake na hivyo kuvuta haiba kubwa machoni mwa watu na kurudi ile hali yake ya awali na hivyo kuthibitisha ule usemi usemao kuwa:- OLD IS GOLD.


KARIBUNI UWELENI SECONDARY SCHOOL

tufuatilie katika mtandao wetu huu http://uwesesco.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment



  • The Members of UWESESCO shall be all students who have been admitted and registered
    to the School at various levels.



  • The active member shall be the one stipulated in the Article No.7 above provided
    that he or she is a full time student.



  • Non active member shall not be entitled to the rights in Article No.9 shall be the one
    who is in one or another fails to attend classes or he/she is not a full time student.



  • The membership retires upon the completion of his or her tenure at UWESESCO.


YALIYOJIRI UWESESCO LEO


 
Support : Masoud Khamis Hamed
Copyright © 2011. Skuli ya Sekondari ya Uweleni - All Rights Reserved