KARIBU UWESESCO - SKULI YA SEKONDARI YA UWELENI; P.O.BOX 100; TEL: +255 24 245 6182; EMAIL: uwesesco@gmail.com ;WEB: http://uwesesco.blogspot.com UWELENI MKOANI PEMBA...
Home » » Milioni 120/ zahitajika kumalizia jengo la Mitihani Skuli ya Uweleni

Milioni 120/ zahitajika kumalizia jengo la Mitihani Skuli ya Uweleni

Na Haji Nassor.

Zaidi ya Shilingi 120 milioni zinahitajika kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo maalum la kufanyia mitihani la ghorofa moja na vyumba vitano vya madarasa, katika Skuli ya Sekondari ya Uweleni Mkoani Pemba.

Akizungumza na Waandishi wa khabari kwa nyakati tofauti Mwalimu anayeshughulikia majenzi Shuleni hapa Maalim Muhammed Ussi Shaame amesema kwa sasa wameshatumia Shilinigi 22 Milioni kwa ajili ya Jiwe la Msingi.

Alisema kati ya fedha hizo walizotumia shilingi 3.5 Milioni ambapo ilikua ni saruji paketi 200, ambao ni msaada kutoka Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Miezi michache iliyopita.

Maalim Ussi alieleza, fedha nyengine walizotumia hadi kufikia hatua hiyo ya msingi ni shilingi 2 milioni kw hatua ya awali kutoka mfuko wa maendeleo wa Jimbo na baadaye Shilingi Milioni 8.

Aidha alisema hata Mwakilishi wa Jimbo la Mkoani Abdallah Muhammed Ali (KILOSA) Amechangia Shilingi 500,000/= katika ujenzi huo unaoendelea Skulini hapa.



Mwalimu huyo anayesimamia ujenzi alifahamisha kuwa, fedha zote hizo hazikukabidhiwa taslimu bali ni vifaa mbali mbali kama vile kokoto, mawe, ndondo na mchanga.

Hata hivyo alisema Waalimu, wazazi wa wanafunzi, nao hawako nyuma katika kuendeleza ujenzi wa jengo hilo, amblo ni agizo la wizara ya Elimu la kila Skuli kuwa na kumbi maalum za kufanyia mtihani.

Alifafanua kuwa, kila mwalimu kwa khiari yake kila mwisho wa mwezi wamekuwa wakichangia shilingi 1500/= pamoja na michango ya miradi midogo midogo ya Skuli.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Skuli hii Maalim Shehe Hassan Moh'd aliwaomba na anaendelea kuwaomba wale wote waliosoma Skulini hapa kuona umuhimu wa kuchangia ujenzi huu ili umalizike kwa wakati.

Akizungumzia mikakati ya kuzipata fedha hizo wanazozihitaji Mwalimu huyo amesema, ni pamoja na kusaka wafadhili kutoka nje.

Mkakati mwengine ni kuwasaka wafadhili wa ndani ikiwa ni pamoja na Wabunge, Wawakilishi na wafanyabiashara wenye nia ya kusaidia na kufikisha kilio chao Serikali kuu.

Idara ya Habari Uwesesco

Share this article :

No comments:

Post a Comment



  • The Members of UWESESCO shall be all students who have been admitted and registered
    to the School at various levels.



  • The active member shall be the one stipulated in the Article No.7 above provided
    that he or she is a full time student.



  • Non active member shall not be entitled to the rights in Article No.9 shall be the one
    who is in one or another fails to attend classes or he/she is not a full time student.



  • The membership retires upon the completion of his or her tenure at UWESESCO.


 
Support : Masoud Khamis Hamed
Copyright © 2011. Skuli ya Sekondari ya Uweleni - All Rights Reserved