Wednesday, 18 March 2015

Tangazo la Nafasi za masomo China

Kuna fursa ya kujiendeleza kimasomo Nchini China, ambapo muombaji anaomba moja kwa moja kupitia mtandao. Zipo fursa katika vyuo mbalimbali, fursa ambazo maelezo yake yajitosheleza ni kwa Chuo cha Beijing Insitute of Technology(BiT) na University of International Business and Economics(UIBE).
Lugha ya kufundishia:
Kiingereza(English) ndio lugha ambayo wanatumia kufundishia, isipokuwa ukihitaji kusoma kwa kichina pia hiyo fursa ipo.

🏤Beijing Insitute of Technology(BiT)
Master's Degree Programs in English:
Electronics and communication Engineering
MBA
Mechanical Engineering
Automatic Control
Software
Doctoral Degree Programs in English
Wasiliana na chuo
🏤University of International Business and Economic(UIBE)
Master's Degree Programs in English:
Accounting
Applied Economics
Finance
International Business
Logistic Management
Law
Finance(Actuarial Science and Risk Management)
International Relations
IMBA”
Doctoral Degree Programs in English
International Economics
Finance
Industrial Economics
Business Management
Law
📍Udhamini(Scholarship) unajumuisha:
Application, tuition, basic learning materials, experiment and internship
Accommodation (on campus or off-campus student dorms)
One-time settlement subsidy: CNY 1,500(USD 245 or Euro 185)
Comprehensive Medical Insurance
Monthly Living allowance:
Master's: CNY 1,700(USD 275, or Euro 210)
Doctorate: CNY 2,000(USD 325, or Euro 245)
Muda wa Masomo
Muda wa masomo Master Degree ni kipindi cha miaka 2-3
Doctoral Degree ni kipindi cha miaka 3-5
📍Vigezo vya kuomba:
Uwe raia wa nchi yeyote lakini sio china
Shahada ya kwanza uweumeipata nje ya china
Kigezo cha Umri usiwe Umezidi Miaka 35 kwa Masters na Doctorate Miaka 40
📍Kusoma Lugha:
Endapo katika kujaza fomu utachagua unahitaji mafunzo ya lugha kabla ya “Major courses”, basi utapata mafunzo ya lugha mwaka mmoja kabla ya kuanza major courses zako. Usipochagua utaanza moja moja “major courses” zako huku ukisoma lugha ya kichina kwa ‘semester’ moja/mbili tu. Unafundishwa lugha yao ili uweze kuwasiliana, lugha kuu ya mawasiliano ni kichina.
📍⚠Jinsi ya kuomba:
▪Jisajili katika mtandao wa scholarship za china ambao nihttp://laihua.csc.edu.cn . Chagua Chinese Government Scholarship kwa aina ya scholarship unayoomba. Wakati wa kujaza ikihitajika Agency Number ya chuo tumia zifuatazo.
Beijing Institute of Technology ni 10007
University of International Business and Economic(UIBE) ni 10036
Ukimaliza hatua zote mpaka mwisho, pakua(download) na ‘print’ hiyo fomu ya maombi. Bandika picha yako katika fomu na jaza taarifa za ziada ambazo hukuzijaza mfano sahihi(signature).
Baada ya hapo ‘scan’ nyaraka zifuatazo Fomu ya Maombi, Advanced Diploma au Degree Certificate, Official copy of Transcript, Study/Research plan(if you have), Photocopy of Passport (including the valid visa page if you are already in China), Recommendation letters from two professors or Lecturers vilevile usisahau kuandaa CV ambayo pia utaituma.

Baada ya hapo tuma hizo document ulizo’scan’ kwa email ukijulisha ni maombi ya kusoma masters:
Beijing Institute of Technology: lq8120@bit.edu.cn copy to master_phd@bit.edu.cn
University of International Business and Economics(UIBE): sie@uibe.edu.cn
Kwa chuo cha UIBE muombaji itabidi aingie katika tovuti yaohttp://english.uibe.edu.cn/ kisha kiungo cha Internatioal Student kisha apply online. Hapo ajisajili kwa kutengeneza akaunti kisha kujaza taarifa zake kupitia akaunti hiyo.
Msimu wa Maombi:
Kuanzia Septemba 1 hadi April 30 kwa kila miaka miwili inayofuatana. Hivi sasa ni 1 Septemba 2014 hadi 30 April 2015
 Angalizo;
i.) Udhamini huu hautoi nauli ya ndege endapo utafanikiwa kuupata. Hivyo gharama zote za huko nyumbani (Tanzania) yaani visa, passport, medical checkup, nauli ya ndege na nyinginezo mpaka unafika China itakuwa ni juu yako. Vilevile ukifika hapa china hakuna kurudishiwa(compensation) gharama ulizotumia katika harakati zote hizo.
ii.) Barua pepe(email) address ambayo utaijaza katika form za maombi unatakiwa uwe na mazoea ya kuifungua mara kwa mara, usitumie ya mtu mwingine.
Mawasiliano yote na chuo baada ya kuwa umepitishwa kupata udhamini yatafanyika kupitia barua pepe yako.
🚦🚦Ushauri:
i.) Ni fursa nzuri kwa anayehitaji kujiendeleza kielimu na hawezi kumudu gharama. Muhitaji yeyote ambaye yupo tayari ajaribu fursa hii kwani utaratibu wa maombi upo wazi. Maombi ni kupitia internet,yanawafikia wahusika moja kwa moja hakuna urasimu.
ii.) Muombaji ambaye amemaliza chuo hivi karibuni tu na bado hajafanikiwa kupata Certificate yake asiwe na hofu anaweza kuanza mchakato wa maombi sasa, katika hatua za awali atatumia Transcript. Pia ambaye hana passport asiwe na hofu kwani si miongoni mwa vigezo vya kupata scholarship, isipokuwa itahitajika baadae wakati ukifika.
iii.) Gharama zote ambazo muombaji atakabiliana nazo(visa($80), passport($75), medical checkup, nauli ya ndege na pesa kujimudu safarini($700) ni takribani USD $900. Ambaye hawezi kumudu na uwezekano wa kuazima upo, basi anaweza kuazima(kukopa) pesa huko nyumbani na akazirudisha taratibu kwani gharama za maisha hapa china zipo chini hivyo kimakisio unaweza ukatumia kiwango cha chini USD $75 au $100 kwa mwezi hivyo ndani ya miezi 5 a 6 utaweza kukusanya USD $ 1000 kutokana na pesa za matumizi unazopewa na kurudisha ulichokopa. Pia gharama hizi ni makadirio ya juu endapo unamiliki passport, ukatumia BIMA yako afya, upande wa ndege ukafanya booking miezi miwili kabla ya safari basi gharama zitapungua.
Ukihitaji maelezo kutoka kwa chuo wasiliana nao:
🏤Beijing Insitute of Technology:
Director International Student: Wany Ying
email :wangying318@gmail.com or yingwang@bit.edu.cn
Graduate Programs Coordinator: Chen Hui
email: master_phd@bit.edu.cn
Tovuti Maalum ya wanafunzi wa kigeni: http://isc.bit.edu.cn
Tovuti ya Chuo: http://english.bit.edu.cn
🏤University of International Business and Economic:
Admissions Office, School of International Education
Email: sie@uibe.edu.cn
Tovuti ya Chuo: http://english.uibe.edu.cn
Excerpt From: Appleseed, John. “Study in China.” iBooks.
This material may be protected by copyright.
TAFADHALI WAPE TAARIFA NA WENGINE

No comments:

Post a Comment